ADSENSE FLOAT CENTER

Tuesday, 4 August 2015

Mke Wa Bobby Brown Akimbizwa Hospitali Baada Kumuaga Bobbi Kristina


 

Mwanamuziki Bobby Brown amezidi kuumia baada ya kuzikwa jana mtoto wake Bobbi Kristina mwenye umri wa miaka 22 na mke wake anayeitwa Alicia Etheredge akikambizwa hospitali baada ya kuzimia.
Ripoti ya TMZ inaeleza, muda mchache baada ya kutoa heshima za mwisho na kuaga kwa Bobbi Kristina, mke wa Bobby Brown amabe juzi kati alijifungua mtoto anayeitwa Bodhi, aliingizwa kwenye gari la wagonjwa (Ambulance) na kukimbizwa hospitali.

 
Lakini, muda sio mrefu Alicia aliweza kurudi kwenye hali yake ya kawaida, Bobby anategemewa kufika kwenye maziko ya Bobbi ambayo yatafanyika New Jersey leo. Bobbi Kristina amefanyiwa misa katika kanisa la St. James United Methodist Church, kanisa alilokuwa akienda kusali na marehemu mama yake Whitney Houston inasemekana kwamba picha ya Whitney Houston ilikuwepo pale.

 
Waombolezaji walitoa mafuriko ya machozi wakati kwaya ikiimba wimbo wa “Stand” ulioimbwa na Donnie McClerkin, wimbo ambao uliimbwa pia wakati wa maziko ya mama yake miaka mitatu iliyopita.
Kwenye mazishi hayo ambayo yalikuwa yakiendelea vizuri, shangazi wa marehemu Bobbi Kristina, Leolah Brown aliombwa aondoke kanisa kufuatia ugomvi uliozuka wakati Pat Houston alipokuwa akitoa heshima za mwisho kwa Bobbi Kristina.

 
Akiongea na maripota nje ya kanisa, Leolah alilalamika kwamba “whitney Houston atakuwa akimfuata Pat Houston kutoka kaburini” kabla hajaenda kutoa heshima kwa marehemu kwa Bobbi Kristina ambaye alikuwa ndani ya jeneza la silva, akiwa anaonekana vry beautiful.

 
Bobbi Kristina alifariki Jumamosi baada ya kukutwa hajijui akiwa ameanguka bafuni kwenye bathtub mwezi Januari.

 
Hali hiyo ya kutojijua alikaa nayo kwa miezi sita, Mungu ailaze roho marehemu mahali pema peponi..Amen.

0 comments:

Post a Comment