ADSENSE FLOAT CENTER

Tuesday, 4 August 2015

Hanscana “Ma-Director wengi wa bongo wanapenda umwinyi”


Director mdogo ambae anafanya vizuri kwa sasa katika game hii ya bongo kwa kufanya video kali na kupelekewa kukubaliwa na wasanii kibao na kutaka kufanya nae video amefunguka na kusema kwamba waongozaji wengi wa muziki hapa bongo wanapenda umwinyi.

Hanscana aliyasema hayo mara baada ya kueleza chance kubwa aliyo ipata wakati wa Director mkubwa kutoka Ghana “Justin Campos” kutimba bongo na kuwaelekeza jinsi yeye anavyofanya kazi na jinsi anavyo jituma licha ya kuwa ni mkubwa kwa maana ya kwamba anafanya vitu ambavyo kwa bongo wengi wamezoea kutumikisha wasaidizi wao na bila kuwapa ujuzi wowote.

0 comments:

Post a Comment