Kama unakumbuka vizuri nyuma kidogo kuliwahi kuibuka na mchuano mkali kati ya Mwanadada Shilole pamoja na Snura Mushi, kwenye game la muziki hapa Tz, ikiwa kipindi hicho ‘Majanga‘ ya Snura ilikuwa imebamba na ‘Nakomaa na Jiji‘ ya Shilole ilikuwa imebamba pia.
Uvumi ukasambaa sana kuwa Shilole na Snura wanabifu, ikaenda ikaendaaa mwishowe zikasambaa nyepesi nyepesi zingine kuwa Snura kamuinulia Shilolemikono, mara baada ya kuonekana amekaa kimya bila kutoa vitu.
Baada ya Snura kujifungua mtoto alirudi na wimbo wa ‘Hawashi’ na kujitetea kuwa ukimya wake ulisababishwa na ujauzito, sasa hivi anategemea kutoa Video mpya ya wimbo unaoitwa ‘Najidabua’
Lakini hii ndio kauli aliyoitoa mara baada ya aliyedaiwa kuwa mpinzani wake maarufu kwa jina la Shilole a.k.aShishibaby or Mrs Nuh kufungiwa muziki na BASATA kwa muda wa mwaka mzima hapa anafunguka zaidi.
” Kwa kweli naamini kuwa Shilole ni mtu mzima kwa kilicho mtokea atakuwa amejifunza nini kinatakiwa na nini hakitakiwi kwenye muziki, nachokiamini mimi, Shilole hawezi kurudia tena makosa coz hilo ni pigo kali sana, ninacho waomba BASATAwangempunguzia adhabu ikabaki hata miezi mitatu au ikiwezekana wamsamehe kabisa” Amesema Snura
0 comments:
Post a Comment