Mwimbaji maarufu wa muziki Bongo, Baraka Da Prince aliyesaini mkataba wa kufanya kazi na label ya Rockstar 4000 mwaka jana 2016, ameamua kuachana na lebo hiyo huku akibainisha sababu za kufanya maamuzi hayo magumu.
Akizungumza leo Julai 21, 2017 kupitia kipindi cha XXL, Baraka amethibitisha kuwa hayupo tena chini ya Rockstar4000 na kuwa anafanya kazi zake binafsi akidai kuna mambo hayapo sawa kati yake na menejimenti huku akisisitiza siyo kwa sababu Alikiba amekuwa mmoja wa wakurugenzi wa label hiyo.
”Kuna vitu lazima uvihoji na ukiona watu unaofanya nao kazi kama kampuni wanakuwa hawajali kitu unachotaka kufahamu kuhusu makubaliano yenu ya kazi inakuwa na mashaka kidogo”
“Naweza kusema sipo chini ya Rockstar kwa sababu mimi ndio boss wa muziki wangu, mimi ndio nafanya kazi, kukiwa na vitu havipo sawa kwa upande wangu mimi ndio naweza kutoa kauli ya mwisho, sipo chini ya Rockstaar”
“Kuna vitu haviko sawa hilo neno boss zito sana, unaponiambia mtu ni boss wangu, how? Boss kivipi kwangu? Alikiba kuwa director wa Rockstar mimi ndio nijitoe, hapana…. kuna vitu havipo sawa na uongozi wa Rockstar”
“Nilipokwenda Rockstar4000 sikusaini chini ya AliKiba, mimi nina matatizo binafsi na uongozi na kama mambo hayapo sawa ukiona kitu jua kipo chini ya Baraka,” alisema Baraka the Prince.
0 comments:
Post a Comment